|
|
|||||||
Alfagems Secondary School - SHERIA ZA SHULEMorogoro Tanzania ALFA = Auto Liberation For Africa |
||||||||
|
ALFAGEMS SECONDARY SCHOOL P.O.Box 6083 – MOROGORO Tel. 0765-899959
/ 0713-784600 www.alfagems.com SHERIA ZA SHULE 1. Sheria za kiutu 1.1.
Uwahi shuleni muda uliopangwa, uwepo muda wote wa masomo na wa kazi
ukifuata ratiba ya shule ndani na nje ya darasa. 1.2.
Uheshimu bendera, picha za viongozi na wimbo wa taifa unaotumiwa na
shule kama sala ya pamoja kila siku; uuimbe umesimama pamoja na kundi
linalokuhusu. 1.3.
Popote ulipo uwe na tabia njema, heshima na utiifu kwa walimu,
wafanyakazi na majirani wa shule, wanafunzi wenzako na binadamu yeyote. 1.4.
Ukifikiwa au kukutana na mwalimu au mtu yeyote anayekuzidi umri usimame
kumsalimia. 1.5.
Ukiitwa na mwalimu yeyote umuitikie mara. 1.6.
Uwe daima safi (mwili, nguo na vitu vyote unavyotumia). 1.7.
Uwe na nywele fupi; usifuge ndevu. 1.8.
Usijirembe kwa kutia nywele dawa, kujichora, kutia wanja n.k. 1.9.
Usiache kucha ndefu wala kupaka rangi au hina. 1.10.
Usivae kofia, jaketi, viatu vya ghorofa wala mapambo yoyote (herini,
bangili, mikufu n.k.). 1.11.
Uvae daima sare ukiwa shuleni (hata wakati wa likizo), ukitoka kwa
shughuli za kishule, ukienda hospitalini, ukisafiri kufika shuleni au kurudi
nyumbani, n.k. 1.12.
Usionekane katika mazingira ya wasiwasi (klabu, kumbi za starehe,
nyumba za wageni n.k.) wala kujihusisha na ulevi na uvutaji wa aina yoyote. 1.13.
Usiwe na urafiki wa kimapenzi; hata hivyo ukipata mimba utakubaliwa
likizo ya uzazi, usije ukaua mimba. 1.14.
Darasani ukae mahali pako, pasipo kuhamahama wala kuchanganyikana na
jinsia nyingine. 1.15.
Uthamini kazi za aina zote na kuzifanya kwa bidii, ukishirikiana na
wenzako katika usafi na utunzaji wa mazingira. 1.16.
Ulinde mali yako binafsi na ya shule (majengo, madawati, vitabu na
vifaa vingine utakavyopewa). 1.17.
Usitoe dawati nje ya jengo lake pasipo agizo au ruhusa. 1.18
Utambue ni marufuku kuiba, kugombana, kupigana, kutumia lugha chafu,
kuchonganisha, kuchochea vurugu na kufanya mgomo. 1.19.
Usitembelee nyumba za walimu na wafanyakazi wengine wala bweni la
jinsia tofauti. 1.20.
Usitoroke shule, bali utoe taarifa kama utashindwa kuhudhuria masomo. 1.21.
Usilete shuleni simu, redio n.k. la sivyo utafukuzwa mara moja. 1.22.
Ukubali mamlaka ya wanafunzi viongozi katika kushauri, kuonya na hata
kuadhibu kabla tatizo lako halijaufikia utawala wa shule. 1.23.
Usikatae adhabu. 2. Sheria za kitaaluma 2.1.
Uwe msikivu na mtekelezaji wa maagizo na mashauri ya walimu. 2.2.
Ukamilishe kazi zote zinazotolewa na walimu kwa wakati unaotakiwa. 2.3.
Uwe mtulivu muda wote darasani, mwalimu awepo au asiwepo vilevile. 2.4.
Ushirikiane vema na walimu pamoja na wanafunzi wenzako ili kupata
msaada wa kitaaluma. 2.5.
Ujitahidi kufanya vizuri mitihani ya mara kwa mara, usije ukaondolewa
shuleni kwa kutoifanya mara tatu mfululizo (hata kama umeruhusiwa kwa shida
maalumu) au kwa kutofikia mara tatu mfululizo wastani wa alama 40.5 kwa masomo
yote. 2.6.
Utambue ni kosa kubwa kuibia, kusaidiwa au kusaidia katika mtihani
wowote. 3. Sheria za nyongeza kwa wanaokaa bweni 3.1.
Uvae sare muda wote uwapo shuleni au bwenini, bila ya kuichanganya na
vazi lingine wala urembo wowote. 3.2.
Kisha kwenda darasani uombe ruhusa ukihitaji kurudi bwenini wakati wa
vipindi. 3.3.
Uzingatie muda wa chakula kwa sababu huruhusiwi kukipeleka bwenini. 3.4.
Usiende nje bila ya ruhusa maalumu; ukienda kwenye ibada uvae sare na
kurudi shuleni mara, bila ya kupitia sehemu nyingine. 3.5.
Usimpokee mgeni yeyote tofauti na walioandikwa na mzazi, wala nje ya
siku za kutembelewa, tena upate kwanza ruhusa ya mkuu wa bweni na usimuingize
bwenini. 3.6.
Usiwasiliane na mtu yeyote bila ya mkuu wa bweni kujua. 4. Adhabu 4.1.
Kwa kosa la kukwepa mtihani wowote, na vilevile la kuibia, kusaidiwa au
kusaidia wakati wa kuufanya, utaandikiwa alama sifuri (0%) katika matokeo yako. 4.2.
Kwa baadhi ya makosa utapewa kwanza maonyo mawili, ambayo yataandamana
na adhabu shuleni na kudai uandike barua ya kukiri kosa na kuahidi hutalirudia. 4.3.
Kwa makosa makubwa zaidi hutapewa maonyo, bali utasimamishwa kwa siku
au wiki kadhaa, kama si kufukuzwa shule. 4.4.
Ukipoteza au kuharibu kitabu au kitu chochote cha shule utatakiwa
kununua kipya na kurejesha, la sivyo hutarudishiwa fedha za tahadhari. 4.5.
Hutarudishiwa vitu visivyotakiwa shuleni vikinyang’anywa na uongozi.
|
||||||||
| Copyright © 2009 Alfagems Co. ltd Morogoro Tanzania | ||||||||