UONGOZI WA SHULE MALENGO YA SHULE MITAALA MAHALI, MAJENGO NA HUDUMA MICHANGO NAFASI ZA MASOMO SHERIA ZA SHULE

   Alfagems Secondary School - Nafazi za Masomo  

 Morogoro Tanzania                                 ALFA = Auto Liberation For Africa

 

ALFAGEMS SECONDARY SCHOOL (S.3874)

S.L.P. 6083 – MOROGORO

Tel. 0765-899959 / 0713-784600

www.alfagems.com

Casella di testo: NAFASI ZA MASOMO

 

 

 

Uongozi wa shule hii,

inayozingatia taaluma na maadili kwa kufuata sera ya elimu ya Kanisa Katoliki,

unawashukuru nyinyi, wananchi wote, kwa kuonyesha mmeipenda sana,

na unafurahi kuwatangazia nafasi zifuatazo:

 

·     KUJIANDAA KWA KIDATO CHA KWANZA (English na Mathematics tu). Masomo yataanza tarehe 21 Septemba 2009 saa 8:00 mchana. Mwisho ni tarehe 18 Desemba 2009. Kufuata masomo hayo hakumpi mwanafunzi haki yoyote ya kuchaguliwa asome kidato cha kwanza baadaye. Ada ni Tsh. 30,000 tu. Wasichana wa bweni wataongeza Tsh. 90,000 tu.

·     KUSOMA KIDATO CHA KWANZA (Civics, History, Geography, English, Kiswahili, Biology, Chemistry, Physics na Mathematics tu). Usaili utafanyika kuanzia saa 2:00 asubuhi tarehe 24-10-2009, 21-11-2009 na 19-12-2009: kila mara watachaguliwa waliofanya vizuri zaidi. Masomo yataanza tarehe 13 Januari 2010 saa 1:30 asubuhi. Ada ni Tsh. 180,000 tu kwa mwaka (mikupuo minne). Wasichana wa bweni wataongeza Tsh. 260,000 tu kwa mwaka (mikupuo minne).

·     KUJIANDAA KWA MTIHANI WA MAARIFA (Q.T. – Civics, History, Geography, English na Kiswahili tu). Masomo yataanza tarehe 19 Oktoba 2009 saa 8:00 mchana (watasoma Jumamosi asubuhi pia). Ada ni Tsh. 160,000 tu kwa mwaka (mikupuo minne). Wasichana wa bweni wataongeza Tsh. 340,000 tu kwa mwaka (mikupuo minne).

·     KUSOMA KIDATO CHA TATU NA CHA NNE KWA MWAKA MMOJA (Civics, History, Geography, English na Kiswahili tu). Wanaotaka kujiunga wanahitaji kuwa wamefaulu mtihani wa maarifa (QT) au wamefanya ule wa kidato cha nne. Masomo yataanza tarehe 19 Oktoba 2009 saa 8:00 mchana (watasoma Jumamosi asubuhi pia). Ada ni Tsh. 160,000 tu kwa mwaka (mikupuo minne). Wasichana wa bweni wataongeza Tsh. 340,000 tu kwa mwaka (mikupuo minne).

·     KUJIANDAA KURISITI MTIHANI WA KIDATO CHA NNE (Civics, History, Geography, English Kiswahili na Bible tu; au Civics, Geography, English, Literature na Kiswahili tu; au Civics, History, Geography, English tu; au History, Geography na Literature tu; au Civics, Kiswahili na Bible tu; au Biology na Mathematics tu). Masomo yataanza tarehe 8 Februari 2010 saa 8:00 mchana (watasoma Jumamosi asubuhi pia). Ada ni Tsh. 100,000 tu kwa mwaka (mikupuo minne). Wasichana wa bweni wataongeza Tsh. 220,000 tu kwa mwaka (mikupuo minne).

·     KUSOMA KIDATO CHA TANO (HKL na HGK). Wanaotaka kujiunga wanahitaji kuwa wamepata tayari credits tatu katika masomo yoyote. Wawe pia wamepata walau D katika somo la English. Masomo yataanza tarehe 12 Aprili 2010 saa 1:30 asubuhi. Ada ni Tsh. 200,000 tu kwa mwaka (mikupuo minne). Wasichana wa bweni wataongeza Tsh. 260,000 tu kwa mwaka (mikupuo minne).

·     KUSOMA KIDATO CHA TANO NA CHA SITA KWA MWAKA MMOJA (HKL na HGK). Wanaotaka kujiunga wanahitaji kuwa na credits tatu tayari katika masomo yoyote walipofanya au kurisiti mtihani wa kidato cha nne. Wawe pia wamepata walau D katika somo la English. Masomo yataanza tarehe 8 Februari 2010 saa 8:00 mchana (watasoma Jumamosi asubuhi pia). Ada ni Tsh. 260,000 tu kwa mwaka (mikupuo minne). Wasichana wa bweni wataongeza Tsh. 340,000 tu kwa mwaka (mikupuo minne).

 

Kwa Wakristo wa madhehebu yoyote somo la Bible Knowledge au la Divinity ni la lazima.

Kwa wengine ni la hiari.

 

Ili kukwepa ulanguzi, fomu za kujiunga zinapatikana hapa tu kwa Tsh. 10,000

na zinakuwa batili wiki moja baada ya masomo kuanza.

 

Ile ya kidato cha kwanza inaweza kununuliwa hata siku ya usaili,

mradi mhusika alete picha yake.

 

Shule haina nafasi katika kidato cha pili, cha tatu, cha nne na cha sita.

 

Tafadhalini, mzingatie taratibu hizi, kwa sababu msongo ni mkubwa mno:

ndiyo sababu tunalazimika kuchuja sana.

 

Kila mtu aelewe kwamba

taaluma inadai idadi ya wanafunzi darasani isizidi kiwango fulani.

 

Kutaka kijana apokewe nje ya taratibu zilizopangwa

ni kuwadhuru kielimu waliokwishakubaliwa.

 

Copyright © 2009 Alfagems Co. ltd Morogoro Tanzania