![]() |
Jimbo
Katoliki la Morogoro |
Mashirika
Vito
mbalimbali katika taji la dhahabu ambalo Kristo amempamba Bibiarusi wake. Au
fungu zuri la maua ya kila rangi. Ni mifano miwili iliyotumika kuelezea wingi wa
mashirika ya kitawa ndani ya Kanisa Katoliki. Jimbo la Morogoro ni mojawapo kati
ya yale yanayofurahia zaidi neema kubwa namna hiyo.
Tukirudi
nyuma hadi karne ya XIX , tunakuta kwamba watawa wa Roho Mtakatifu (Holy Ghost
Fathers) ndio waanzilishi wenyewe wa Kanisa nchini, wakitokea Zanzibar na
Bagamoyo, na kufuatwa muda si mrefu baadaye na masista kutoka kisiwa cha Réunion
(Filles de Marie) Hivyo tangu awali watawa wamekuwa mstari wa mbele sio tu
katika maisha ya Kiroho, bali pia katika umisionari.
Mwanzo
mgumu: kwa miaka mingi mashirika hayo yaliinjilisha wakistahimili tabu na hari
za mchana, mpaka watawa wengine hasa wananchi, tunda la kazi yao, wakaja
kuwaunga mkono kwa saa tofautitofauti.
Masista
wengi wa nchi nzima wanafahamu sana jimbo hili kwa sababu waliwahi kusoma Bigwa,
katika sekondari iliyoanzishwa kwa ajili yao na Umoja wa Mama Wakuu Tanzania (ambao
kwa sasa unakamilisha ujenzi wa kituo kingine cha malezi ya pamoja si mbali na
shule hiyo).
Hatua
mpya ya uwepo wa mashirika jimboni ilipigwa pale ambapo Wasalvatoriani kisha
kupatana na mashirika mengine walichagua Morogoro kama mahali pa kujenga
seminari kuu ya kitawa ambayo kwa sasa ni Taasisi ya Falsafa na Tauhidi (wengine
wanafikiria kuigeuza tena iwe Chuo Kikuu chenye vitivo mbalimbali). Hayati
Askofu Adriani Mkoba alifungua milango ya jimbo kulipokea kila shirika
litakalohitaji watawa wake wasomee huko. Tangu hapo ujenzi na malezi havijakoma
katika eneo la mlima Kola, kwenye barabara ya Dar es Salaam. Yeyote anayepita
anajionea maendeleo hayo na kuzungumzia aina hiyo ya Vatikano chini ya milima ya
Uluguru.
Mvuto
wa taasisi hiyo ndio sababu kuu ya mashirika kumiminika Morogoro miaka ya mwisho;
lakini ukianza kuelekea Dodoma, kwenye eneo la Kihonda unakuta vilevile
mashirika mengi, ingawa majengo yao yamefichikafichika kati ya nyumba za
wananchi.
Kwa
jumla sasa hivi jimbo lina mashirika zaidi ya 30 ya kila aina: ya wanaume na ya
wanawake, ya kikleri na ya kilei, ya maisha ya wakfu na ya maisha ya kitume, ya
kipapa na ya kijimbo. Inakosekana bado monasteri ya maisha ya sala tu, ingawa
Askofu Telesphor Mkude ana hamu nayo.
Mhashamu
akiona kwa furaha kubwa ongezeko hilo ambalo linaendelea haraka, mwanzoni mwa
Jubilei kuu ya mwaka 2000, pamoja na kumteua kwa mara ya kwanza makamu wake
maalumu kwa maisha ya wakfu aliamua kuunganisha mashirika hayo yote katika
ASSICAL (Association of Institutes of Consecrated and Apostolic Life –
Morogoro Diocese) ili yaweze kufahamiana na kubadilishana mawazo, mang’amuzi,
matarajio na mipango hasa upande wa malezi na wa utume.
Tangu
hapo utume huo unazidi kuimarika kwa njia ya mikutano na adhimisho la pamoja la
sikukuu ya watawa iliyoanzishwa na Papa Yohane Paulo II kwenye tarehe 2 Februari
ya kila mwaka. Kwa kweli ni tukio la kufurahisha kuona mamia ya watawa wa mabara
karibu yote kushangilia miito yao mbalimbali kwa ajili ya ufalme wa mbinguni.
Lakini siku moja haiundi mwaka. Kuna siku nyingine 364 ambazo ni nafasi ya kila
mtu kumshukuru Mungu kimatendo kwa karama aliyomjalia. Uaminifu wa kila sasa
ndio unaothibitisha kwamba neema inapokewa kwa mikono miwili badala ya kuchezewa.
La sivyo adhimisho halina maana. Changamoto hiyo ipo daima mbele ya kila mmoja
na ya kila jumuia, kwa sababu maisha ya kitawa ni ya kulenga utakatifu pamoja na
wengine, sio kibinafsi.
Mbali
ya utakatifu, mashirika yanalenga kutoa mchango katika Kanisa na katika jamii,
kila moja kadiri ya karama yake. Ingawa nguvu nyingi za mashirika mbalimbali
yaliyohamia jimboni kwa ajili ya malezi zinaishia katika kazi hiyo ya msingi,
tunaweza kusema nia ya kufanya kitu hata nje ya nyumba ipo. Kadiri ushirikiano
unavyostawi, njia zinaonekana, kwa sababu penye nia pana njia.
Mahitaji
ya jimbo hasa ni mengi, kama kawaida. Hivyo mapadri na walei wanatazamia sana
kufaidika na uwepo wa umati huo wa waamini wenzao waliojitoa kabisa kwa maisha
ya wakfu na ya kitume. Baadhi ya mashirika yana nyumba zisizo za malezi, nazo
ndizo zinazoitikia zaidi mahitaji hayo. Kwa namna ya pekee Masista wa Moyo Safi
wa Maria wa Morogoro, ambao ndio wengi, wanahudumia parokia, shule na zahanati
nyingi jimboni kote.
Mungu
atujalie sisi sote kushika kwa unyenyenyeku nafasi aliyotupangia katika
kufikisha watu kwenye uzima wa milele.
1.
MASHIRIKA YA MAISHA YA WAKFU
1.1.
Mashirika ya Kitawa
1.1.1. Ya Kiume
1.
Ndugu
Wafransisko Wakonventuali - SLP 932 - Morogoro Simu: +023/0784594072 - Barua pepe: krzcie@yahoo.com
- Tovuti: www.ofmconv.org 2.
Ndugu
Wafransisko Wakapuchini - SLP 900 - Morogoro Simu:
+023/2603204 - Barua pepe: kolafriars@yahoo.com
- Tovuti: www.ofmcap.org 3.
Ndugu Waagustino - SLP 1947 - Morogoro Simu:
+023/2604773 - Barua pepe: osamorogoro@yahoo.com
- Tovuti: 4.
Wakarmeli OCD - SLP 363 - Morogoro Simu:
+023/2603800 - Barua pepe: ocdtzmission@yahoo.com
- Tovuti: 5.
Shirika la Roho Mtakatifu - SLP 16 - Bagamoyo Simu:
+023/2440063 - Barua pepe: eap@habari.co.tz
- Tovuti: 6.
Wamisionari wa
Mt. Francis wa Sales - SLP 12 - Morogoro Simu:
+023/2600036 - Barua pepe: msfsmoro@africaonline.co.tz
- Tovuti: www.fransalians.com 7.
Shirika la Madonda Matakatifu (Wastigmatini) - SLP 2213 - Morogoro Simu:
+023/2603523 - Barua pepe: stigmatines@morogoro.net
- Tovuti: www.stigmatines.com 8.
Wamisionari Wana wa Moyo Safi wa Maria (Waklareti) - SLP 427 - Morogoro Simu:
+023/2600429 - Barua pepe: cmfmorobarbastro@yahoo.com
- Tovuti: www.claret.org 9.
Wasalvatoriani - SLP 1878 - Morogoro Simu:
+023/2600897 - Barua pepe: sdsschol@go2.pl
- Tovuti: http://www.sds-ch.ch/africa 10.
Wamisionari wa Consolata - SLP 769 - Morogoro Simu:
+023/2603563 - Barua pepe: allasemi@morogoro.net
- Tovuti: http://www.consolata.org 11.
Shirika la Misheni (Wavinsenti) - SLP 6051 - Morogoro Simu:
+023/2600029 - Barua pepe: depaulmoro04@yahoo.com
- Tovuti: 12.
Mabradha wa Elimu ya Kikristo wa Mt. Gabrieli (Wamontfort) - SLP 1124 -
Morogoro Simu: +023/2602204 -
Barua pepe: montmoro@africaonline.co.tz -
Tovuti: 1.1.2. Ya Kike
1.
Mabinti wa
Maria (wa St. Denis)- SLP 230 - Bagamoyo Simu:
023/2440417 - Barua pepe: dmdestdenistan@yahoo.fr
- Tovuti: 2.
Masista Wamisionari wa Damu Takatifu - SLP 865 - Morogoro Simu:
+023/2604655 - Barua pepe: - Tovuti: 3.
Shirika la Moyo Safi wa Maria (wa Morogoro) - SLP 1049 - Morogoro Simu:
+023/2603591/2604314 - Barua pepe: mgololesisters@intafrica.com
- Tovuti: 4.
Masista wa Msalaba Mtakatifu (wa Chavonod)- SLP 1677 - Morogoro Simu:
+023/2603328 - Barua pepe: holycross@africaonline.co.tz
- Tovuti: 5.
Masista Watersiari Wakapuchini wa Familia Takatifu - SLP 1989 - Morogoro Simu:
+023/2604845 - Barua pepe: htctanz@hotmail.com
- Tovuti: 6.
Masista wa Mt. Anna (wa Luzern) - SLP 1807 - Morogoro Simu:
+023/2601550 - Barua pepe: stannsmoro@africaonline.co.tz
- Tovuti: 7.
Masista Wakolejina wa Familia Takatifu - SLP 945 - Morogoro Simu:
+023/2600424 - Barua pepe: collemoro@hotmail.com
- Tovuti: 8.
Masista wa Maria Imakulata (wa Krishnagar) - SLP 2028 - Morogoro Simu:
+023/2604066 - Barua pepe: smimoro@africaonline.co.tz
- Tovuti: 9.
Masista wa Mama wa Karmeli - SLP 1302 - Morogoro Simu: +023/2600359 -
Barua pepe: - Tovuti: 10. Masista wa Mt. Gemma
- SLP 304 -
Morogoro- Simu: +0784/457358
- Barua pepe: - Tovuti: 11.
Masista Waursula wa Yesu Mteswa - SLP 1048 - Morogoro Simu: +0756/937297 -
Barua pepe: - Tovuti: 12. Masista wa
Sakramenti Kuu - SLP 2135 - Morogoro Simu: +023/2602902 -
Barua pepe: - Tovuti: 13.
Mabinti wa Mt. Fransisko wa Sales – SLP 640 - Morogoro Simu: +023/2600900 -
Barua pepe: dsfstanzania@rediffmail.com
- Tovuti: 14. Masista wa Maria
Imakulata (wa Wroclaw) - SLP 1878 - Morogoro Simu: +0787/759496 -
Barua pepe: - Tovuti: 15. Masista wa Mt.
Yosefu (wa Annecy) - SLP 58 - Dumila Simu: +0745/214343 -
Barua pepe: agnesadampukulam@yahoo.com -
Tovuti: www.sisters of st.joseph of Annecy 16. Masista wa Mt.
Yosefu (wa Chambery) - SLP 135 – Mikumi Simu: +0787/710338 -
Barua pepe: - Tovuti: www.csjchambery.org 17. Masista wa Bikira
Maria Malkia wa Mitume - SLP 1925 - Morogoro Simu: +023/2604165 -
Barua pepe: - Tovuti: 18. Masista wa Mt. Anna
(wa Bangalore) – SLP 363 – Morogoro Simu: +023/603800 -
Barua pepe: - Tovuti: 19. Masista Waabuduo
Damu ya Kristo – SLP 6508 – Morogoro Simu: - Barua pepe: -
Tovuti: 20. Dada Wadogo wa Mt.
Fransisko – SLP 1878 – Morogoro Simu: +0787/759496 -
Barua pepe: - Tovuti: 21. Masista Wabenedikto
Waafrika wa Mt. Agnes – SLP 6015 – Morogoro Simu: +0784/464024 -
Barua pepe: mlowevicky@yahoo.com - Tovuti: 22. Masista wa Mt.
Karolo Borromeo – SLP 1232 – Morogoro Simu: +0732/931181 -
Barua pepe: - Tovuti: 23. Masista Warosmini wa
Maongozi – SLP 133 – Morogoro Simu: +0787/024621 -
Barua pepe: - Tovuti: 1.2.
Mashirika ya Kilimwengu
1.2.1. La Kiume
1.
Mapadri wa
Shirika la Kilimwengu katika Kazi ya Roho Mtakatifu – SLP 640 – Morogoro Simu: +023/2603340 -
Barua pepe: - Tovuti: 1.2.2. Ya Kike
1.
Unitas kwa Afrika - SLP 1003 - Morogoro Simu:
+023/2600138 - Barua pepe: - Tovuti: 2.
Masista wa Grail - SLP 6090 - Morogoro Simu: +023/2613690 -
Barua pepe: - Tovuti: 2. MASHIRIKA YA
MAISHA YA KITUME
2.1. Ya
Kiume
1.
Wamisionari wa Damu Azizi - SLP 1925 - Morogoro Simu:
+023/2604165 - Barua pepe: stgascoll @yahoo.com
- Tovuti: www.cpps-preciousblood.org 2.
Jumuia ya Mapadri katika Kazi ya Roho Mtakatifu - SLP 1935 - Morogoro Simu: +023/2601353 -
Barua pepe: - Tovuti: 2.2. La Kike
1.
Jumuia ya Masista katika Kazi ya Roho Mtakatifu - SLP 6038 - Morogoro Simu: +023/2601764 -
Barua pepe: - Tovuti: 3.
TAASISI ZA MALEZI YA PAMOJA KATI YA MASHIRIKA YA KIKE 1.
Sekondari ya Masista ya Bigwa - SLP 369 - Morogoro Simu:
+023/2603066 - Barua pepe: bigwasrs@yahoo.com
- Tovuti: 2.
Kituo cha Malezi ya Masista cha Kola – SLP 913 – Morogoro Simu: +023/2600658 -
Barua pepe: tcastanzania@hotmail.com -
Tovuti: 4.
CHAMA (CHA WANAUME NA WANAWAKE) 1.
Ndugu Wadogo wa Afrika - SLP 6083 - Morogoro Simu: - Barua pepe: unwa@unwa.tk
Tovuti: www.unwa.tk 1.
INSTITUTES OF CONSECRATED LIFE
1.1.
Religious Institutes
1.1.1. Of men
1.
Friars Minor
Conventual - P.O.Box 932 - Morogoro Phone: +023/0784594072 -
E-mail: krzcie@yahoo.com - Website: 2.
Friars Minor
Capuchin - P.O.Box 900 - Morogoro Phone: +023/2603204 - E-mail: kolafriars@yahoo.com
- Website: 3.
Augustinian
Friars - P.O.Box 1947 - Morogoro Phone: +023/2604773 - E-mail: osamorogoro@yahoo.com
- Website: 4.
Discalced
Carmelites - P.O.Box 363 - Morogoro Phone: +023/2603800 - E-mail: ocdtzmission@yahoo.com
- Website: 5.
Holy Ghost
Fathers- P.O.Box 16 - Bagamoyo Phone: +023/2440063
- E-mail: eap@habari.co.tz
- Website: 6.
Missionaries of
St. Francis of Sales - P.O.Box 12 - Morogoro Phone: +023/2600036 - E-mail: msfsmoro@africaonline.co.tz
- Website: www.fransalians.com 7.
Stigmatines -
P.O.Box 2213 - Morogoro Phone: +023/2603523 - E-mail: stigmatines@morogoro.net
- Website: www.stigmatines.com 8.
Claretians -
P.O.Box 427 - Morogoro Phone: +023/2600429 - E-mail: cmfmorobarbastro@yahoo.com
- Website: www.claret.org 9.
Salvatorians - P.O.Box 1878 - Morogoro Phone: +023/2600897 - E-mail: sdsschol@go2.pl
- Website: http://www.sds-ch.ch/africa 10. Missionaries
of Consolata - P.O.Box 769 - Morogoro Phone: +023/2603563 - E-mail: allasemi@morogoro.net
- Website: http://www.consolata.org 11. Congregation
of Mission (Vincentians) - P.O.Box 6051 - Morogoro Phone: +023/2600029 - E-mail: depaulmoro04@yahoo.com
- Website: 12. Montfort
Brothers of the Christian Instruction of St. Gabriel - P.O.Box 1124 - Morogoro Phone:
+023/2602204 - E-mail: montmoro@africaonline.co.tz
- Website: 1.1.2. Of women
1.
Daughters of
Mary (of St. Denis)- P.O.Box 230 - Bagamoyo
Phone: +023/2440417 - E-mail: dmdestdenistan@yahoo.fr - Website: 2.
Missionary
Sisters of the Precious Blood - P.O.Box 865 - Morogoro Phone: +023/2604655 - E-mail: - Website: 3.
Immaculate
Heart of Mary Sisters (of Morogoro) - P.O.Box 1049 - Morogoro Phone: +023/2603591/2604314 - E-mail: mgololesisters@intafrica.com
- Website: 4.
Holy Cross
Sisters (of Chavonod)- P.O.Box 1677 - Morogoro Phone: +023/2603328 - E-mail: holycross@africaonline.co.tz
- Website: 5.
Capuchin
Tertiary Sisters of the Holy Family - P.O.Box 1989 - Morogoro Phone: +023/2604845 - E-mail: htctanz@hotmail.com
- Website: 6.
Sisters of St.
Ann (of Luzern) - P.O.Box 1807 - Morogoro Phone: +023/2601550 - E-mail: stannsmoro@africaonline.co.tz
- Website: 7.
Collegine
Sisters of the Holy Family - P.O.Box 945 - Morogoro Phone: +023/260424 - E-mail: collemoro@hotmail.com - Website: 8.
Sisters of Mary
Immaculate (of Krishnagar) - P.O.Box 2028 - Morogoro Phone: +023/2604066 - E-mail: smimoro@africaonline.co.tz
- Website: 9.
Sisters of
Mother of Carmel - P.O.Box 1302 - Morogoro Phone:
+023/2600359 - E-mail: - Website: 10.
Sisters of St. Gemma - P.O.Box 304 -
Morogoro- Phone:
+0784/457358 - E-mail: - Website: 11.
Ursuline Sisters of the Agony of Jesus - P.O.Box 1048 - Morogoro Phone:
+0756/937297 - E-mail: - Website: 12.
Blessed Sacrament Sisters - P.O.Box 2135 - Morogoro Phone: +023/2602902
- E-mail: - Website: 13. Daughters
of St. Francis de Sales - P.O.Box 640 - Morogoro Phone: +023/2600900 - E-mail: dsfstanzania@rediffmail.com
- Website: 14. Sisters
of Mary Immaculate (of Wroclaw) - P.O.Box 1878 - Morogoro Phone: +0787/759496
- E-mail: - Website: 15. Sisters
of St. Joseph (of Annecy) - P.O.Box 58 - Dumila Phone: +0745/214343
- E-mail: agnesadampukulam@yahoo.com
- Website: www.sisters of st.joseph of
Annecy 16. Sisters
of St. Joseph (of Chambery) - P.O.Box 135 - Mikumi Phone: +0787/710338
- E-mail: - Website:
www.csjchambery.org 17. Sisters
of Mary Queen of the Apostles - P.O.Box 1925 - Morogoro Phone:
+023/2604165 - E-mail: - Website: 18. Sisters
of St. Ann (of Bangalore) - P.O.Box 363 - Morogoro Phone: +023/603800
- E-mail: - Website: 19. Adorers
of Blood of Christ - P.O.Box 6508 - Morogoro Phone: -
E-mail: - Website: 20. Little
Sisters of St. Francis of Assisi - P.O.Box 1878 - Morogoro Phone: +0787/759496
- E-mail: - Website: 21. African
Benedictine Sisters of St. Agnes - P.O.Box 6015 - Morogoro Phone: +0784/464024
- E-mail: mlowevicky@yahoo.com - Website: 22. Sisters
of St. Charles Borromeo - P.O.Box 1232 - Morogoro Phone: +0732/931181
- E-mail: - Website: 23. Rosminian
Sisters of Providence - P.O.Box 133 - Morogoro Phone: +0787/024621
- E-mail: - Website: 1.2.
Secular Institutes
1.2.1. Of men
1.
Secular
Institute of Priests in Opus Spiritus Sancti - P.O.Box 640 - Morogoro Phone: +023/2603340
-
E-mail: - Website: 1.2.2. Of women
1.
Unitas for
Africa - P.O.Box 1003 - Morogoro Phone: +023/2600138 - E-mail: - Website: 2.
The Grail -
P.O. Box 6090 - Morogoro Phone: +023/2613690
- E-mail: - Website: 1.
SOCIETIES OF APOSTOLIC LIFE
2.1. Of men
1.
Missionaries of the Precious Blood - P.O.Box 1925 - Morogoro Phone:
+023/2604165 - E-mail: stgascoll @yahoo.com -
Website: www.cpps-preciousblood.org 2.
Apostolic Life Community of Priests in Opus Spiritus Sancti - P.O.Box
1935 - Morogoro Phone:
+023/2601353 - E-mail: - Website: 2.2. Of women
1.
Apostolic Life
Community of Sisters in Opus Spiritus Sancti - P.O.Box 6038 - Morogoro Phone:
+023/2601764 - E-mail: - Website: 3.
INTERCONGREGATIONAL CENTRES OF FORMATION FOR SISTERS 1.
Bigwa Sisters’ Secondary School - P.O.Box 369 - Morogoro Phone:
+023/2603066 - E-mail: bigwasrs@yahoo.com -
Website: 2.
Kola Sisters’ Holistic Formation Centre - P.O.Box 913 - Morogoro Phone: +023/2600658
-
E-mail: tcastanzania@hotmail.com
- Website: 4.
ASSOCIATION (OF MEN AND WOMEN) 1.
Little Brothers
and Sisters of Africa - P.O.Box 6083 - Morogoro Phone: - E-mail: unwa@unwa.tk - Website: www.unwa.tk. |
|