Jimbo Katoliki la Morogoro Jiografia

   

  Hali ya Kijiografia  

-         Jimbo Katoliki la Morogoro limeundwa na eneo lipatalo kilomita za mraba 43,380 kusini mashariki mwa Jamhuri ya Tanzania. Jimbo la Morogoro limeundwa kutokana na Wilaya za Serikali tano, yaani Morogoro Mjini, Morogoro Vijijini, Kilosa, Mvomero, na Bagamoyo. Wilaya ya Bagamoyo ni sehemu ya Mkoa wa Pwani Kiserikali, wakati Wilaya nne zilizobaki zipo katika Mkoa wa Morogoro.

-         Makao Makuu ya Mkoa wa Morogoro yapo katika Manispaaa ya Morogoro. Vile vile katika Manispaa hii yanapatikana Makao Makuu ya Jimbo la Morogoro, Kanisa Kuu la Jimbo, na Makao ya Askofu wa Jimbo.  

Wakazi wa Jimbo  

-        Jimbo la Morogoro lina wakazi wapatao 1,559,271.  Kati ya hao wakatoliki ni 638,591.

-         Ni asilimia ishirini (20%) tu ya wakazi wa Jimbo la Morogoro wanaishi mijini, wakati asilimia kubwa, yaani 80%, wanaishi vijijini.

-  Makabila asilia yanayopatikana Jimboni Morogoro ni Waluguru, Wanguu, Wakutu, Wazigua,  Wakami, Wakaguru, Wavidunda, Wasagara, Wakwavi, Wakwere, Wazaramo na Wadoe,

-         Mbali ya makabila haya asilia, Jimbo la Morogoro lina wahamiaji vile vile. Makundi haya ya wahamiaji wengi wao ni Wachaga, Wamasai, Wangoni na Wagogo.

-         Kila kabila lina lugha yake ya asili. Hata hivyo, Kiswahili kinatumika katika sehemu zote katika Jimbo la Morogoro.