UONGOZI WA SHULE MALENGO YA SHULE MITAALA MAHALI, MAJENGO NA HUDUMA MICHANGO NAFASI ZA MASOMO SHERIA ZA SHULE

Alfagems Second. School            Mitaala       Morogoro Tanzania                                 ALFA = Auto Liberation For Africa

Asubuhi shule yetu inafuata mitaala iliyotolewa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (kidato cha kwanza hadi kidato cha sita), kwa kuzingatia imani na maadili ya Kanisa Katoliki, pamoja na mila njema za Watanzania ili nchi iweze kujengwa kwa uimara.

Masomo ya Bible Knowledge na Divinity ni ya lazima kwa Wakristo wote.

Aidha, masomo ya Dini yanafundishwa kadiri ya imani ya wanafunzi na utayari wa walimu wa kujitolea kutoka dini husika

Lugha ya Kiingereza ndiyo itakayotumika kufundishia kwa kuzingatia maelekezo ya Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi

Shule yetu ni ya sekondari kuanzia kidato cha 1 hadi cha 6. Kuanzia mwaka 2010 asubuhi kutakuwa na mikondo 24 (6x4) .

Shule yetu inapokea hata watu waliochelewa kupata elimu (wanandoa, wafanyakazi n.k.), madarasa yanatumika hata jinni na Jumamosi kwa kozi za haraka kuliko kawaida.

Kwa hiyo, mikondo inaweza kuwa 48, na wanafunzi wote 2160.Kwa sasa wasichana 400 wanaishi katika mabweni ya shule, wengine na wavulana wote wanatokea nyumbani.


Copyright © 2009 Alfagems Co. ltd Morogoro Tanzania