Maisha na utendaji |
![]() |
Wakiwa
viumbe na watoto wa Mungu, wanaofurahi kumtegemea kabisa, ndugu wadogo
wanatafuta katika sala uso wake na matakwa yake, pamoja na nguvu ya kuyatekeleza.
Ratiba
ya jumuia ina walau dakika 250 za sala, zilizogawanyika kati ya usiku na mchana
ili ziongoze mwendo wa maisha ya kila siku, zikimuachia kila mmoja nafasi
nyingine za kuongea na Baba kwa njia ya Mwana katika Roho Mtakatifu.
Maisha
ya Kiroho yanazaa ushirika wa kidugu na utendaji wa nje: nyakati za kusoma,
kufanya kazi na kuburudika kwa uwiano wa kufaa.
Masomo
yanahusu kwanza kabisa Neno la Mungu, ambalo ndio msingi wa malezi ya awali na
ya kudumu, na ambalo linaangaza mambo yote na namna ya kuyakabili kwa hekima.
Kazi
zinajumlisha zile za mikono kwa ajili ya mahitaji ya jumuia na ya fukara, zile
kwa ajili ya ustawi wa jamii (ushauri nasaha kwa familia, kituo cha kulelea
watoto wadogo, shule ya kompyuta, sekondari isiyotoza ada yoyote), na hasa zile
za uinjilishaji (katika parokia, jumuia ndogondogo za Kikristo, madarasa, redio,
wiki za uamsho kwa vijiji vya mbali).
Sikukuu
na burudani za kijumuia (mbili kwa siku) ndiyo nafasi ya kuacha furaha ya kuwa
ndugu ilipuke na ya kuchanga kwa upendo imani na maisha.
|
Majukumu
ya kila siku |
MALEZI Safari
ya kila mmoja kuelekea ukomavu, kwa
kuongozana na waliomtangulia na jamaa nzima, inayohitajika
ili upendo usibaki neno tupu, bali
ufikie ukamilifu. |
SALA Fungamano
na Mungu, lililo
hamu ya dhati zaidi moyoni mwa binadamu, la
kustawishwa kwa makusudi na uangalifu na
mtu mmoja mmoja na jumuia pia, ili
lizae matunda ya uzima wa milele. |
KAZI Tunu
ya kudumishwa katika ulimwengu wa starehe, juhudi
kwa utekelezaji wa chochote kinachohitajika au kinachomfaa mtu, inazidi
kuwa na maana ikipangwa na kufanywa kwa pamoja, kadiri
ya matakwa ya Baba. |
|
Majukumu
ya kila siku |
MALEZI Safari ya kila mmoja kuelekea ukomavu, kwa kuongozana na waliomtangulia na jamaa nzima, inayohitajika ili upendo usibaki neno tupu, bali ufikie ukamilifu. |
SALA Fungamano
na Mungu, lililo
hamu ya dhati zaidi moyoni mwa binadamu, linalostawishwa
kwa makusudi na uangalifu na
mtu mmoja mmoja na jumuia pia, ili
lizae matunda ya uzima wa milele. |
KAZI Tunu
ya kudumishwa katika ulimwengu wa starehe, juhudi
kwa utekelezaji wa chochote kinachohitajika au kinachomfaa mtu, inazidi
kuwa na maana ikipangwa na kufanywa kwa pamoja, kadiri ya matakwa ya Baba. |