Karama ya pekee kwa ajili ya mpango wa Baba
Jina
lenyewe la chama linaonyesha kuwa karama maalumu ni ile ya Kifransisko ya udugu
na udogo ikiwa na uhusiano wa pekee na bara la Afrika.
Kwanza
kabisa Roho Mtakatifu anawajalia wanachama, kidogo kama alivyomjalia mtakatifu
Fransisko wa Asizi, kumtazama kwa namna ya pekee Yesu, Mwana wa Baba, katika
kujishusha moja kwa moja kwa ajili yetu.
Kwa
kuwa yeye kwa upendo na unyenyekevu amejifanya ndugu na mtumishi wetu, wao pia
kwa upendo na unyenyekevu wanajisikia mvuto wa kuishi kama ndugu wadogo wa wote,
hasa wa watu wa mwisho, ambao wanafanana zaidi na Mwana wa Mtu aliyeteswa.
Tangu
karne nyingi Afrika ni kielelezo cha mtu kudhulumiwa na mwenzake, jambo la aibu
lililochapwa kwa dhati katika saikolojia ya umati.
Mlio
wa maskini wake, ambao hausikilizwi na wakuu wa ulimwengu huu, unazingatiwa na
Mungu hata kwa kuwatuma ndugu wadogo wa kiume na wa kike ambao wawainamie
majeraha ya roho na ya miili yao ili kuwaelekeza kwenye uhuru wa wanae.
Sharti la kuwaokoa Waafrika kwa njia
ya Waafrika ni kutamadunisha kwa dhati ujumbe wa Injili na maisha yaliyowekwa
wakfu kwa njia ya useja mtakatifu, ufukara na utiifu, hata viwe na maana na
manufaa katika hali halisi ya maisha yao yalivyo leo.
Mshikamano, jina jipya la amani.
Ukweli
usiopingika wa kwamba binadamu wote ni ndugu unadai tuishi kidugu, tusikubali
tofauti kubwa mno kati ya hali za maisha.
Katika
ulimwengu uliojaa maonevu, ni lazima tushikamane na wanyonge, kwa mfano wa Yesu,
Mwana wa Mungu aliyejifanya fukara kwetu sisi sote, lakini hasa kwa ajili yao.
Kwa
ndugu wadogo wa Afrika mshikamano huo maana yake sio tu kutaka kuwasaidia fukara,
kama toka juu, bali kushiriki iwezekanavyo mateso na matumaini yao.
Wito
huo wa kuwa jirani kabisa na watu wa mwisho ndio unaoathiri zaidi ufukara wao
halisi katika chakula, mavazi, makao, matumizi ya vyombo vya mawasiliano na
mengineyo yote.
Nguzo
za utawa
-
USEJA
MTAKATIFU.
Nguvu
ya kupenda iliyo maalumu ya moyo safi,
ulio
tayari daima kujitoa na kumtumikia yeyote,
usiotawaliwa
kamwe na umimi wa tamaa,
ulio lengo la kulikazania kwa makusudi,
ili
kuzaa matunda mengi zaidi.
-
UFUKARA.
Uhuru
wa kimaisha
unaotokana
na kuchagua moja kwa moja mema ya milele,
na
kujiaminisha kwa tumaini mikononi mwa Mungu,
na
kushikamana kabisa na watu wa mwisho,
wale
ambao hawana hata vitu vya lazima.
-
UTIIFU.
Msimamo
wa msingi wa Mwana wa Mungu,
wa
kuweka pembeni matamanio yake
ili
kutambua na kutekeleza mpaka mwisho
mpango
wa upendo wa Baba kwa faida ya ndugu wote.
|