Historia

 

Izazi: La prima Cappella - Izazi: Kikanisa cha kwanza - Izazi: The first chapel

Home Karama Historia Maisha na utendaji Katiba Safari ya Malezi Maktaba Pepe 

Historia kwa ufupi (ya jana na ya kesho)

 

Ndugu Wadogo wa Afrika walianza kukusanyika tarehe 4-10-1991 kwenye kijiji cha Izazi (mkoa wa Iringa, nchini Tanzania), halafu wakahamia Mkungugu (mkoa huohuo) na kuanzia tarehe 31-10-1995 katika mtaa mmojawapo wa mji wa Morogoro.

 

Muda wa jaribio ulimalizika tarehe 9-7-1997, askofu Telesphor Mkude wa Morogoro alipounda rasmi chama chao pamoja na kuthibitisha katiba yake.

 

Wakati wa adhimisho la ekaristi waanzilishi 11 (6 wa kike na 5 wa kiume) waliweka ahadi ya kuishi kijumuia Injili kadiri ya Kanuni ya Utawa Hasa wa Tatu wa mtakatifu Fransisko, iliyothibitishwa na papa Yohane Paulo II, na kadiri ya katiba hiyo maalumu.

 

Baada ya nyumba asili mbili, ziliongezeka ile ya kiume ya Kiroka (27-1-1998), ile ya kike ya kijiji hichohicho (15-9-1998) na ile ya kiume ya Langali (10-7-2000), zote zikiwa katika mkoa wa Morogoro.

Tangu tarehe 4-11-2004  wameanza kuwepo hata Kapelekesi katika jimbo la Mbeya, mipakani kwa Malawi.

Mnamo tarehe7 Januari 2007 waliowekwa wakfu kwa ahadi ya daima walikuwa 11 (6 wa kiume na 5 wa kike), wanachama wenye ahadi ya muda walikuwa 17 (5 kwa 12), na ndugu kwenye jaribio 16 (6 kwa 10).

Hamu kuu ya ndugu hao ni kumshuhudia Yesu kwa maneno na kwa maisha yao yote, katika Afrika nzima na mpaka miisho ya dunia, kwa kuwa kila mtu anamhitaji yeye, mwokozi wa ulimwengu, na kwa hiyo ana haki ya kumjua ili awe kitu kimoja naye na Baba aliyemtuma.

 

Kwa ajili hiyo wanatarajia kupata mapema Wafransisko wa ulimwenguni, hasa wenye ndoa, ambao washuhudie tunu zilezile za kwao katika maisha ya kila siku ya watu wa kawaida: katika familia, uchumi, siasa n.k.

 

Ndugu Wadogo wa Afrika wamejiunga na Baraza la Kifransisko la Kimataifa la Utawa Hasa wa Tatu (International Franciscan Conference of the Brothers and Sisters of the Third Order Regular).