|
Jina |
NDUGU Umoja
wa kidugu ni mang’amuzi matamu lakini ya nadra: unawezeshwa
tu na upendo ule ambao Yesu aliuishi mpaka mwisho akatushirikisha
katika Roho wake. Ni
jambo la kutekelezwa kwa wote na katika ngazi zote, katika
hali halisi ya maisha ya kila siku, kwa
furaha ya Baba yetu sote. |
WADOGO Hata
katika ulimwengu wa G8, wa
wenye uwezo wanaofanya lolote wanalotaka, inawezekana
kujichagulia maisha ya wadogo, kama alivyofanya Fransisko wa Asizi. Kwa
sababu kilicho kidogo ni kizuri, kwa
kuwa Mungu amejifanya mdogo, ili
kusimama upande wa watu wa mwisho, na
kushikamana na wale wanaoshindwa katika ushindani wa kimataifa. |
WA
AFRIKA Bara
asili la binadamu wote, labda
kwa sababu hiyo linavutia kuliko yote. Ni
nchi ya watu wanaodhulumiwa tangu zamani, wenye
tunu nyingi za kiutu za kuweza kushirikisha, lakini
wametupwa pembeni kwa historia na uchumi wa kimataifa. Limegeuzwa
kuwa jalala isiyo na mipaka, mgodi
wa kushindaniwa, soko
kubwa la kuuzia bidhaa. |
||
|
|
Lebo |
|
|||
|
|
Chama, kilichoanza wakati wa
upapa wa Yohane Paulo II, kinafuata Kanuni aliyowathibitishia ndugu wa
kiume na wa kike wa Utawa Hasa wa Tatu wa mtakatifu Fransisko. Zaidi ya hayo, kimechota kwa
wingi katika maisha yake ya Kiroho yaliyozama ndani ya fumbo la Kristo na
Maria na kujitokeza katika ngao yake ya kipapa yenye herufi M (yaani Maria)
chini ya msalaba. Kwa hiyo wanachama wanavaa saa
zote kanzu ya Kifransisko ambayo upande wa moyo ina lebo inayotumia ishara
hizohizo juu ya ramani nyeusi ya Afrika. Bara hilo, ambalo pengine lina
hali ngumu kiasi cha kutisha, linatawaliwa tayari tena italibidi lizidi
kutawaliwa na msalaba wa Kristo, mwekundu kwa damu na kama moto wa Upendo
wa Mungu unaotakiwa kupamba duniani kote. Chini yake, M nyeupe
linamaanisha moyo safi wa Maria, uliomwezesha kutazama kwa dhati na
kushiriki kikamilifu mpango wa Mungu ulipotimia katika sadaka ya utiifu wa
Mwanae kwa wokovu wa binadamu wote. Lebo ni mwaliko na hamu ya kuwa
wana halisi wa Maria, wenye moyo safi wa kimama kama wa kwake mbele ya
msalaba wowote ambao Yesu anaendelea kuteseka ndani ya wale aliowaita
ndugu zake wadogo, akitangaza kwamba mwishoni tutahukumiwa kuhusu yale
yote ambayo tumemtendea au kuacha kumtendea kila mmojawao. |
|
|||
| KATIBA YA UTAWA WA NDUGU WADOGO WA AFRIKA (9/7/1997) |