Visitor:  Hit Counter

The Tanzania National Anthem

UNWA
Info
Stralci dalle Circolari (Raccolti dal compianto Enrico Riccioni)
Circolare 44

Ndugu Wadogo wa Afrika ni wanaume na wanawake Wafransisko wamisionari wa Kanisa Katoliki wenye makao makuu mjini Morogoro (Tanzania).

Cha kwao ni chama cha maisha yaliyowekwa wakfu kwa Mungu kwa njia ya ahadi ya kushika mashauri ya Kiinjili ya useja mtakatifu, ufukara na utiifu kadiri ya utamadunisho safi wa karama ya udugu na udogo waliyorithi kwa mtakatifu Fransisko wa Asizi.

Mtindo wa maisha yao unakusudiwa kumfuata Yesu kwa kutekeleza kijumuia Injili yake na kushikamana na watu wa leo walio fukara zaidi ili uwe habari njema kwao na kwa wale wote wanaotamani dunia ijae haki, amani na upendo.

Wakiamini kwamba hiyo itabaki ndoto ya mchana tu ikiwa wanaume na wanawake watajaribu kuujenga kwa nguvu zao wenyewe, Ndugu Wadogo wa Afrika wanaikimbilia sala usiku na mchana kusudi uhusiano na maongezi na Baba wa wote vizijalie akili furaha ya ukweli, viunganishe mioyo, vitakase na kuimarisha ndani ya kila mmoja nia ya kutumikia kwa ukarimu wenye shida kubwa zaidi na viwafanye wote kuwa vyombo vya amani yake.

Roho Mtakatifu, tunayeshirikishwa kwa njia ya Yesu mteswa, mzikwa na mfufuka, ndiye anayegeuza hivyo kila mmoja na wote kwa jumla ili kuwafanya kwa pamoja mashahidi wa Kristo hadi mipaka ya mwisho ya dunia.

Tangazo la jina lake, la maisha yake, la msalaba wake mtukufu, la fumbo lake na la mafundisho yake ndiyo huduma kuu wanayoweza kuwapatia ndugu zao katika ubinadamu.

Hilo linaendana na mipango ya kuendeleza watu na vitendo vidogovidogo vya kila siku ambavyo wanawashirikisha waliyojaliwa na mikono ya Mungu kwa njia ya kazi zao au kwa misaada ya watu wengine waliosogezwa jirani na utandawazi.

Ndugu Wadogo wa Afrika, wakijua kwamba wanachoweza kufanya ni kidogo kweli, wanatia maanani ushirika na viungo vyote vya familia ya Mungu, yaani Kanisa linaloongozwa na Papa na Maaskofu wenzake: ndani yake mchango wao mdogo kwa ustawi wa utawala wa Mungu unaweza kuwafaidisha wengi, kwa sababu upendo unazidishwa na uenezi wake.

Upendo huo unatakiwa kupamba kama moto ili kufuta aina yoyote ya ubinafsi na umimi inayowafunga watu ndani yao wenyewe na ya faida zao, ikiwafanya sio tu wasiweze kuzaa lolote bali waharibu maisha yao na ya wenzao, unavyothibitisha utamaduni wa Magharibi ambao umegeuka utamaduni wa kifo.

Kinyume chake, wao wanataka kudumisha, kustawisha na kueneza tunu bora za makabila ya Afrika ili wachangie utamaduni wa uhai na wa mshikamano usio na mipaka.

Ni kwa Maria, mama wa Yesu, kwamba wanataka kujifunza unyenyekevu wapokee neema ya moyo safi wenye kuwaka upendo ili kumshangilia Mungu na kumtumikia kila mtoto wake.  

The Little Brothers and Sisters of Africa are Franciscan missionaries of the Catholic Church with base in Morogoro (Tanzania).

This is an association of life consecrated to God through the promise to observe the evangelical counsels of chastity, poverty and obedience according to a genuine enculturation of the charisma of fraternity and minority, which they have inherited from st. Francis of Assisi.

Their way of life aims at following Jesus through the fulfillment of his Gospel, all together and in solidarity with the most poor of the today world, so to become good news for them and for all the people who hope a world of justice, peace and love.

Believing that it will remain only a hopeless dream if men and women try to build it by themselves, the Little Brothers and Sisters of Africa run to the prayer day and night so that the assiduous contact and dialogue with the common Father may give to their minds the joy of the truth, unity of  hearts, purify and strengthen in all the intention of serving generously the most in want, and make them instruments of his peace.

It is the Holy Spirit, shared by Jesus dead and risen, who does transform anyone and all in such a way to turn them into Christ’s witnesses up the last boundaries of the earth.

The proclamation of his name, his life, his glorious cross, his mystery and his teaching is the best service they may offer to their brothers and sisters in humanity.

It is accompanied by works of human promotion and by little everyday deeds of sharing what they have received from God’s hand through their own work or contributions from people made nearby by the globalization.

The Little Brothers and Sisters of Africa, knowing that what they can do is really something very little, valorize the communion with all the members of God’s family, i.e. the Church guided by the Pope and his fellow Bishops: in unity with  it, their little contribution for the growing up of God’s kingdom may help many people, because the love, while spreading, does multiply itself.

It is a love blazing like fire, to eliminate any form of individualism and egotism which closes a person in himself and his profits, and so make him not only sterile but also harmful to himself and to others, as shown by the today western culture, which has become a culture of death.

On the contrary, they want to conserve, develop and diffuse the best values of the African peoples, in order to contribute to the establishment of a culture of life and solidarity at a global level.

It is from Jesus’ mother, Mary, that they want to learn the humility, to be able to receive the gift of a pure heart burning of love,  exulting in God and serving every child of him.  

I Piccoli Fratelli e Sorelle d’Africa sono francescani missionari della Chiesa Cattolica con base in Morogoro (Tanzania).

La loro è un’associazione di vita consacrata a Dio tramite la promessa di osservare i consigli evangelici di castità, povertà ed obbedienza secondo una sana inculturazione del carisma di fraternità e minorità ereditato da san Francesco di Assisi.

La loro forma di vita si propone di seguire Gesù con la pratica comunitaria del suo Vangelo in solidarietà coi più poveri di oggi così da essere una buona notizia per essi e per tutti quelli che anelano ad un mondo di giustizia, pace ed amore.

Credendo che esso resterà solo un sogno se gli uomini e le donne cercheranno di costruirselo con le proprie forze, i Piccoli Fratelli e Sorelle d’Africa ricorrono alla preghiera giorno e notte perché l’assiduo contatto e colloquio col Padre comune doni alle menti la gioia della verità, unisca i cuori, purifichi e rafforzi in tutti l’intenzione di servire generosamente i più bisognosi, e ne faccia strumenti della sua pace.

E’ lo Spirito Santo, comunicato tramite Gesù morto e risorto, a compiere tale trasformazione di ognuno e di tutti per renderli insieme testimoni di Cristo fino agli estremi confini della terra.

L’annunzio del suo nome, della sua vita, della sua croce gloriosa, del suo mistero e del suo insegnamento costituisce il massimo servizio che possono rendere ai loro fratelli e sorelle in umanità.

Ad esso si affiancano opere di promozione umana e piccoli gesti quotidiani di condivisione di quanto ricevuto dalla mano di Dio attraverso il proprio lavoro o i contributi di gente resa vicina dalla globalizzazione.

I Piccoli Fratelli e Sorelle d’Africa, coscienti che quanto possono fare è veramente poco, valorizzano la comunione con tutti i membri della famiglia di Dio, la Chiesa guidata dal Papa e dai suoi colleghi Vescovi: in essa il loro piccolo contributo alla crescita del Regno di Dio può riuscire di vantaggio a tanti, perché l’amore diffondendosi si moltiplica.

E’ un amore che deve divampare come il fuoco per eliminare ogni forma di individualismo e di egoismo che chiude in sé stessi e nei propri interessi, rendendo non solo sterili ma dannosi a sé e agli altri, come dimostra la cultura occidentale divenuta una cultura di morte.

Al contrario, essi vogliono conservare, sviluppare e diffondere i migliori valori dei popoli africani per contribuire ad una cultura della vita e della solidarietà globale.

E’ da Maria, la madre di Gesù, che vogliono imparare l’umiltà per accogliere il dono di un cuore puro ed ardente di amore per esultare in Dio e servire ogni suo figlio.

 

Links:

Franciscan Web Page

Franciscan Experience

Franciscans International (deutsch, espanol, francais,italiano, english)

Missionary Agency [italiano,

english, francais]

Catholic Directory

EWTN (english, espanol)

Library (italiano, espanol, francais, deutsche)

faith questions

New Advent

 

The Holy Bible (English, Italian, French, etc)

Concilium Vaticanum

John Paul II

Benedict XVI

Catechism of the Catholic Church (english, francais,deutsch, italiano, latin, espanol)

Compendium of the Catechism of the Catholic Curch  (French, Italian, Romanian)

Catholic Almanac

The Hierarchy of the Catholic Church

Ecclesiatic Library